Home »
» UCHAMBUZI MGOGORO WA AFGHANISTAN
UCHAMBUZI MGOGORO WA AFGHANISTAN
Wachambuzi wanasema mgogoro wa Afghanistan unaweza kuwa mbaya zaidi duniani kuliko hata wa Syria, wakati vurugu zikiendelea miaka 17 tokea uvamizi uliongoozwa na Marekani. Graeme Smith, mshauri wa Kimataifa wa Kundi linaloshughulikia Migogoro, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba baadhi ya dalili zinaonyesha kuwa vita vya Afghanistan vinaweza kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20,000 mwaka huu pekee, ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida na wapiganaji. Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imeonyesha kwamba vita vya Afghanistan vineshasababisha vifo vya raia wapatao 1,692 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu.
Solomoni tv
0 comments:
Post a Comment