Wazimbabwe wajitayarisha kwa uchaguzi Jumatat
Wasafiri wa kawaida waliobeba mahindi, mablanketi na sabuni za kufulia walikaa pamoja na wapiga kura wakielekea nyumbani kwa ajili ya uchaguzi wa kwanza nchini Zimbabwe tangu kiongozi aliyeongoza nchi hiyo kwa mkono wa chuma Robert Mugabe kuondolewa madarakani miezi minane iliyopita.
Mabehewa sita ya treni hiyo iliondoka katika kituo kikuu cha mjini Johannesburg cha Central Park mapema jioni ya Ijumaa katika safari ya masaa 15, ya kilometa 600 katika majira haya ya baridi.
"Watu wa Zimbabwe wanahitaji maisha mapya ili waweze kusahau juu ya maisha magumu tuliyopitia chini ya yule mzee Mugabe," amesema abiria mmoja Emile Manyikunike, mwenye umri wa miaka 36, akivalia koti la baridi la ngozi lenye rangi nyeusi na fulana ya kijani yenye picha ya Bob Marley.
"Watu walikuwa wanapigwa na polisi kwa kutokubaliana na serikali, na hata hatukuweza kuwaamini majirani zetu kwasababu kila mtu wa pili alikuwa ni mpelelezi wa ZANU-PF," aliliambia shirika la habari la AFP.
SolomoniTv
SolomoniTv
0 comments:
Post a Comment