Watu watano wameuawa leo baada ya mripuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu katika wilaya ya Hodan. Hayo yamesemwa na polisi. Afisa wa polisi Ali Hassan ameliambia shirika la habari la Ujerumani DPA, kuwa gari lililojazwa mabomu liligonga malango ya makao makuu ya kiutawala ya wilaya hiyo na kuwaua maafisa watatu wa polisi. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini linafanana na mashambulizi mengine ambayo hufanywa na kundi la Kiislamu la al-Shabaab ambalo mara kwa mara hushambulia taifa hilo lililokumbwa na msukosuko.
Solomoni tv
0 comments:
Post a Comment