Solomonitv brog ni Brog ya kisasa itakayo kuhabarisha habari zote katika Dunia hii,Kwa matangazo zaidi husisite kuwasiliana nami maana Bei ni nafuu sana habari whatsapp No +255 624 499 969 Au +255 759 290 764

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa


Guterres atoa wito mapigano yasitishwe Idlib
saa (0) nyuma
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kusitishwa mapigano katika mji wa Idlib, huku operesheni ya majeshi ya serikali ya Syria wakisaidiwa na mashambulizi ya anga ya Urusi ikiendelea.
Guterres amezitaka pande zote zinazohusika katika vita hivi kuwalinda raia, lakini akiweka msisitizo zaidi kwa wale aliowaita wafadhili watatu wa mchakato wa Astana - mazungumzo yaliyoanzia katika mji mkuu wa Kazakhstan; Urusi na Iran, ambayo wanaomuunga mkono Rais Bashar al Assad na Uturuki inayowaunga mkono waasi.

"Idlib haifai kugeuzwa kuwa eneo la umwagikaji damu. Hatua hiyo itasababisha matatizo makubwa ya kibinaadamu ambayo hayajawahi kutokea katika migogoro nchini Syria. Vita dhidi ya magaidi haviziondolei pande husika majukumu yake chini ya sheria ya kimataifa."

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, takribani watu elfu thelathini wamelazimika kuyakimbia makaazi yao makwao mwezi huu kutoka Idlib kufuatia mapigano hayo. Urusi na Syria awali zilitetea hatua za kuwapeleka wanajeshi wao nchini Syria kwa kusema kwamba wanawalenga magaidi.

Hapo jana, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan De Mistura, alikutana na maafisa wa Urusi, Iran na Uturuki katika juhudi za kupata uungaji mkono wa kuanzisha mazungumzo ya amani kati ya pande zinazotofautiana nchini Syria.  Hayo yakijiri, Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amekataa kuondosha uwezekano wa Ujerumani kuanzisha mashambulizi dhidi ya Syria iwapo serikali ya nchi hiyo itatumia silaha za kemikali kwa waasi eneo la Idlib, lakini akasisitiza kwamba watafanya uamuzi huo kwa uhuru.
Solomoni tv

Share:

0 comments:

Post a Comment