Rais Donald Trump wa Marekani amewasili nchini Uingereza tayari kwa ziara yake ya kwanza akiwa rais, wakati ambapo kuna wasiwasi ndani ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO, maandamano na sintofahamu katika mchakato wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya ama Brexit.
Trump aliwasili jijini London ambako ataanzia ziara yake ya siku nne nchini humo. Atahudhuria pia hafla ya chakula cha jioni pamoja na maafisa wa Uingereza na Marekani baadaye leo. Hapo kesho, Trump atakutana na Waziri Mkuu Theresa May na Malkia Elizabeth. Kunatarajiwa maandamano makubwa kote nchini humo wakati wa ziara yake, inayokuja katika wiki ngumu kwa serikali ya May, inayowania kuanza tena mazungumzo ya Brexit.
Solomoni TV
0 comments:
Post a Comment