Solomonitv brog ni Brog ya kisasa itakayo kuhabarisha habari zote katika Dunia hii,Kwa matangazo zaidi husisite kuwasiliana nami maana Bei ni nafuu sana habari whatsapp No +255 624 499 969 Au +255 759 290 764

Ofisi ya rais nchini Nigeria imesema inapanga kutumia njia ya mazungumzo ili kuwezesha kuachiliwa huru kwa wasichana wa shule 110 waliotekwa


Ofisi ya rais nchini Nigeria imesema inapanga kutumia njia ya mazungumzo ili kuwezesha kuachiliwa huru kwa wasichana wa shule 110 waliotekwa katika mji wa Dapchi, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo mwezi uliopita, badala ya kutumia nguvu za kijeshi.

Utekaji huo ndio mkubwa zaidi tangu kundi la Boko Haram lenye itikadi kali ya Jihadi, lilipowateka wasichana 270 wa shule katika mji wa Chibok mwaka 2014. Baadhi ya wasichana hao wameachiliwa huru baada ya kile vyanzo vya habari vya kiusalama vimesema ni kutokana na fidia kulipwa. Takriban wasichana 100 hawajaachiwa huru .

Ofisi ya rais wa Nigeria imeeleza kuwa Nigeria ingependa kuwapata wasichana waliotekwa Chibok na Dapchi wakiwa hai.
Solomoni tv
Share:

0 comments:

Post a Comment