Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeutaka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO kuondoka ifikapo 2020. Waziri wa mambo ya nje Leonard She Okitundu amesema hayo baada ya kura ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya wiki iliyopita ya kuuongezea mamlaka ujumbe huo kwa mwaka mwingine.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mzozo nchini humo umekuwa mbaya zaidi, wakati raia wa Kongo milioni 13.1 wakihitaji misaada ya kiutu, ikiwa ni pamoja na milioni 7.7 wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha kwa kauli moja azimio lililowasilishwa na Ufaransa la kuuongeza mamlaka ujumbe wa MONUSCO hadi Machi 2019, na kusisitiza umuhimu wa kuwalinda raia katika wakati ambapo taifa hilo linaelekea katika uchaguzi wa kihistoria mwezi Desemba.
Solomoni tv
0 comments:
Post a Comment