idadi ya watu waliokufa imeongezeka hadi kufikia 127
Idadi ya watu ambao wamefariki dunia kutokana na ajali ya kivuko MV Nyerere imeongezeka hadi 127
Idadi ya watu ambao wameaga dunia kufuatia ajali ya feri MV Nyerere nchini Tanzania, imeongezeka na kupita watu 127
Waokozi wanaendelea na shughuli zao kutafuta manusura au miili ya watu wanaohofiwa wamefariki.
Kwa mujibu wa ripoti kwenye vyombo vya habari nchini humo, wakati kilipopinduka majini, huenda chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria 200, kiasi ambacho ni maradufu ya kiwango kinachostahili kubeba.
Walioshuhudia wanasema MV Nyerere ilizama wakati abiria walipokimbilia upande mmoja kushuka ilipokaribia kutia nanga.
Tangaza na solomoni tv
Kwa mujibu wa mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania Simon Sirro aliyenukuliwa na idhaa inayomilikiwa na serikali TBC Taifa, idadi ya watu waliokufa imeongezeka hadi 127
Solomoni tv
Umoja wa Ulaya wakataa mapendekezo ya May kuhusu Brexit
Uingereza na Umoja wa Ulaya wameshindwa kufikia makubaliano kuhusu mchakato wa nchi hiyo kujiondoa - Brexit. Sababu zilizokwamisha mazungumzo ni suala la mpaka wa Ireland na uhusiano wa kibiashara wa siku zijazo.
Uingereza ikiwa inatarajiwa kujitoa katika Umoja wa Ulaya Machi 29 mwakani, kuna wasiwasi kwamba makubaliano juu ya uhusiano wa kibiashara wa baadae huenda yasifikiwe katika muda uliopangwa.
Viongozi wote, akiwamo Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May wanatafuta njia ya kutatua suala zito kuhusu mchakato wa Brexit ambalo ni jinsi ya kuhakikisha bidhaa zinaendelea kuingizwa na kutoka kati ya Ireland Kaskazini ambayo ni sehemu ya Uingereza na Jamhuri ya Ireland ambayo ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Wakati walipokutana kwa siku mbili katika mkutano wa kilele uliomalizika jana mjini Salzburg Austria, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk amesema baadhi ya sehemu za mpango wa May wa Brexit - uliopewa jina la Chequers -hazitokubalika.
"Wakati wa kudhihirika ukweli kuhusu makubaliano ya Brexit utakuwa katika Baraza la Umoja wa Ulaya la mwezi Oktoba. Oktoba tunatarajia maendeleo ya kiwango cha juu na makubaliano katika mazungumzo ya Brexit," amesema Donald Tusk.
Solomoni tv
SHUGULI ZA UOKOAJI ZINAENDEDEA
Shughuli za uokozi zimeanza tena kuwatafuta wahanga wa ajali feri ya MV Nyerere ambayo ilipinduka Alhamis katika Ziwa Victoria, Tanzania. Watu 37 waliokolewa wakiwa hai. Rais Magufuli amepeleka salamu za rambirambi.
Idadi ya watu ambao wamefariki dunia nchini Tanzania kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichopinduka jana Alhamis katika Ziwa Victoria, imeongezeka na kufikia watu 86. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti kwenye gazeti la kibinafsi nchini humo Citizen. Hapo awali kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali nchini humo kiliripoti kuwa idadi ya vifo iliongezeka hadi 79, kikimnukuu mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella. Hadi jioni ya jana, waokozi walikuwa wameweza kuwapata watu 37 wakiwa hai, haya yakiwa ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mogella. Kulingana na taarifa za maafisa wa Tanzania, idadi ya vifo inatazamiwa kuongezeka na juhudi za uokozi zinaendelea.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, na kuwatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa. Wakala wa Ufundi na Umeme unaohusika kusimamia chombo hicho umewataka wananchi kuwa na subira katika taarifa yake huku juhudi za uokozi zikiwa zimeshaanza.
Kupakia kupita uwezo
Shirika hilo limesema kivuko hicho kilikuwa kinatoka Ukara na kuelekea Bugolora na kilizama karibu na Mwanza. Mwandishi wa DW aliyeko Mwanza, akimnukuu mkuu wa wilaya ya Ukerewe Colnel Magembe, amesema kivuko kilichopata ajali kilikuwa kikibeba abiria zaidi ya uwezo wake, kwa sababu ingawa kinatakiwa kupakia wasiozidi 100, kilipopata ajali kilikuwa kimejaza abiria zaidi ya 300.
Amesema wakati kivuko hicho kikikaribia kwenye bandari ndogo ya Bwisa, watu wengi walitaka kushuka kwa wakati mmoja, wakajazana mbele na kusababisha uzito wote sehemu moja, na hivyo kusababisha kuzama.
MADA ZINAZOHUSIANA
Hali hiyo ya msongamano katika kivuko hicho, amesema Bulendu, hujitokeza hasa siku ya Alhamis kwa sababu ya mnada unaofanyika siku hiyo kwenye soko la Bwisa kisiwani Ukara.
Matukio ya mara kwa mara
Ajali za vyombo vya majini ni tukio la mara kwa mara katika maziwa ya Tanzania na Uganda, mara nyingi zikitokana na uchakavu wa vyombo hivyo, au kupakia abiria na mizigo kupita uwezo.
Mwaka 1996, ajali mbaya zaidi iliyohusisha meli ya MV Bukoba iliuwa watu wasiopungua 800 katika ziwa hilo la Victoria.
Mwaka 2011, ajali nyingine mbaya ya meli ya MV Spice Islander ilizama katika Bahari ya Hindi karibu na pwani ya Zanzibar, na kuuwa watu zaidi ya 200.
Solomoni tv
Baada ya kuachiwa huru mwanasiasa Mkongwe Nchini Rwanda
Kiongozi wa chama cha upinzani cha FDU-Inkinge, nchini Rwanda bibi Ingabire Umuhoza Victoire ameachiwa huru mwishoni mwa wiki kutokana na amri ya rais Paul Kagame. Katika mahojiano na DW bibi Ingabire Victoire ameelezea matumaini ya kuiona Rwanda ikifungua milango kwa vyama vyengine vya kisiasa.
Katika mahojiano hayo na DW mwenyekiti wa chama cha Front Democratic Un ifié-FDU Inkinge, Ingabire Umuhoza Victoire amezungumzia jinsi alivyostaajabishwa na uamuzi wa kumuachia huru na kusema: "Bila ya shaka nilishangaa kwa sababu nilipata habari usiku na sikuweza kulala kwasababu sikuelewa kama ningeachiwa huru haraka."
Bibi Ingabire alikuwa atumikie kifungo cha miaka 15 jela. Akielezea jinsi hali ilivyokuwa jela kiongozi huyo wa chama cha FDU anazungumzia shida alizokutana nazo miaka mitano ya mwanzo ambayoanasrema ilikuwa migumu kwangu kwasaabu alikuwa amefungwa peke yake na hakuwa na mtu yeyote wakuzungumza nae.Na miaka mitatu ya mwisho lakini alitumikia kifungo pamoja na wafungwa wengine kwa hivyo angalao alikuwa na watu wakuzungumza nao.
Milango ya kisiasa imeanza kufunguka Rwanda?
Katika mahojiano yake na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa huru Jumamosi iliyopita, bibi Ingabire alisema anahisi milango ya kisiasa imeanza kufunguka hivi sasa nchini Rwanda. Hoja hiyo ameitoa alipohojiwa na DW aliposema:
MADA ZINAZOHUSIANA
"Nimesema hivyo kwasababu nimeona wiki zilizopita chama cha Green kwa mfan o kiliruhusiwa bungeni na wiki mbili baadae nikaachiwa huru. Na mnatambua akwamba serikali imeniachia huru katika wakati ambapo chama achangu cha kisiasa kimetangaza nimechaguliwa tena kukiongoza chama hicho. Kwa hivyo serikali inatambua kwamba mie ndie kiongozi wa chama katika upande wa upinzani. Ikiwa wamekubali kuniachia huru,nahisi wanajaribu kufungua miango ya kisiasa nchini Rwanda. Na nnataraji watafanya mengi zaidi kwasababu kuna viongozi wengine wa vyama vya kisiasa walioko jela kama mnavyojua."
Solomoni tv
UCHAMBUZI MGOGORO WA AFGHANISTAN
Wachambuzi wanasema mgogoro wa Afghanistan unaweza kuwa mbaya zaidi duniani kuliko hata wa Syria, wakati vurugu zikiendelea miaka 17 tokea uvamizi uliongoozwa na Marekani. Graeme Smith, mshauri wa Kimataifa wa Kundi linaloshughulikia Migogoro, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba baadhi ya dalili zinaonyesha kuwa vita vya Afghanistan vinaweza kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20,000 mwaka huu pekee, ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida na wapiganaji. Ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa imeonyesha kwamba vita vya Afghanistan vineshasababisha vifo vya raia wapatao 1,692 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu.
Solomoni tv